Nkupamah media:
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi
Mh.Mwigulu Nchemba akisalimiana na Rais wa Vietnam NdgTruong Tan Sang
mapema hii leo walipokutana kwaajili ya mazungumzo kuhusu fursa zilizopo
katika kilimo,mifugo na uvuvi katika nchi mbili hizi rafiki
Katika mazungumzo ya pamoja kati
ya Rais wa Vietnam na Mh.Mwigulu Nchemba na ujumbe wake,Pande hizi mbili
zimekubaliana kushirikiana kwenye uzalishaji wa mbegu bora za mazao na
uzalishaji wa samaki hapa nchini,Mbali zaidi wamekubaliana kufungua
fursa zaidi kwa wafanyabiashara wa nchi hizi mbili kuwekeza kwenye
kilimo,mifugo na uvuvi.
Mauzungumzo yakiendelea kati ya ujumbe kutoka Vietnam na wadau wa kilimo hapa nchini.
Mh.Mwigulu Nchemba akiagana na Rais wa Vietnam mara baada ya mazungumzo ya pamoja kumalizika.
Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.


0 comments :
Post a Comment