Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad
Masauni(kushoto), akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Kassim Majaliwa alipotembelea Kambi ya Utenganisho ya
Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera, kambi hiyo inahifadhi
wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi ya wakimbizi kutoka nchini
Burundi kwa sababu za kiusalama.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa(kushoto),
akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya wakimbizi,iliyoko chini ya Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke. Waziri Mkuu alitembelea
Kambi ya Utenganisho ya Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera,
kambi hiyo inahifadhi wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi ya
wakimbizi kutoka nchini Burundi kwa sababu za kiusalama.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa(kushoto),
akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya wakimbizi,iliyoko chini
ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Selemani Mziray. Waziri Mkuu
alitembelea Kambi ya Utenganisho ya Mwisa,iliyoko wilayani
Misenyi,mkoani Kagera, kambi hiyo inahifadhi wakimbizi waliotengwa
kutoka katika makambi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi kwa sababu za
kiusalama.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa,akizungumza na
Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani), wakati
alipotembelea kambi ya Utenganisho ya Mwisa iliyoko wilayani Misenyi,
mkoani Kagera. kambi hiyo inahifadhi wakimbizi waliotengwa kutoka katika
makambi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi kwa sababu za
kiusalama.Katikati Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Mwigulu Nchemba na
kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad
Masauni.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad
Masauni(kushoto), akimuongoza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Kassim Majaliwa(wa pili kulia) kwenda kuongea na wakimbizi
waliohifadhiwa katika kambi ya Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani
Kagera.Anayefuatia baada ya Waziri Mkuu ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza nchini, John Minja na wa mwisho ni Mkuu wa Magereza mkoa wa
Kagera, SACP Omari Mtiga.
(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)


0 comments :
Post a Comment