Tokeo la picha la easter images
Leo ni siku ya Pasaka ambapo Wakristo Duniani kote wanasheherekea siku hii muhimu ikiwemo kulitukuza jina la Bwana Yesu Kristo maana yeye alifanyika kuwa mwanakondoo kwa ajili ya ukombozi wake ili wanaadamu tuokolewe kutoka katika dhambi kama nukuu za vitabu takatifu (1 Korintho 5 : 7) Inavyoelekeza
Hivyo uongozi mzima wa mtandao pendwa wa Nkupamah media  unapenda kuwatakia heri ya Pasaka na pia unatoa rai kwa Jamii nzima kuhakikisha wanazingatia suala la amani na usalama wa mali zao hasa majumbani na sehemu watakazokuwa katika kusheherekea siku hii ya leo.
Tujiepushe na matumizi ya vileo kupita kiasi, tusiendeshe vyombo vya moto kwa kasi, pia familia zenye watoto wadogo wasiwaruhusu watoto wao waende kutembea bila waangalizi ilikuepuka matatizo yanayokuwa yanajitokeza mara kwa mara kama ilivyotokea siku  za hivi Karibuni Maeneo tofauti ya Nchi yetu
Endelea kusoma mtandao wako bora wa Nkupamah media kwa habari mbali mbali za kila siku popote ulimwenguni tunakujuzi Kwa wakati