Hilo pia limemtokea Rais wa Real Madrid, Florentino Perez alipokuwa akitoa hutoba yake katika kumbukumbu ya nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi na Barcelona, Johan Cruyff ambaye alifariki Ahlamisi huku chanzo cha kifo chake kikitajwa kuwa ugonjwa wa Saratani.
Perez alisema Cruyff alikuwa mmoja wa watu ambao alikuwa akifata nyayo zao katika soka na anaamini kama kuna watu hawakustahili kufa, Johan Cruyff ni mmoja wapo.
“Hizi ni siku za huzuni, nina amini kama kuna watu hawakustahili kufa na Johan Cruyff ni mmoja wapo,
“Tulizaliwa mwaka mmoja na nimekuwa nikimfuatilia kwa maisha yake yote, alibadili historia ya Barcelona na soka kwa ujumla, na sio Hispania peke yake hata dunia nzima, ni mmoja wa watu ambao historia zao zitadumu milele,” alisema Perez.