Waziri
wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa ametoa pongezi
kwa kampuni mpya ya simu ya Halotel kwa juhudi zake inazofanya katika
kutekeleza mkakati wa kuhakikisha huduma ya mawasiliano inapatikana
maeneo ya vijijini.
Pamoja
na ongezeko la zaidi ya asilimia 16 la idadi ya watumiaji wa simu za
mikononi nchini bado tatizo la upatikanaji wa huduma ya mawasiliano kwa
maeneo ya vijijini imekuwa ni changamoto.
Prof
Mbarawa alisema serikali imekuwa inafanya juhudi mbalimbali ili kuziba
pengo la upatikanaji wa huduma ya mawasiliano kati ya maeneo ya vijijini
na mijini, na hivyo mwaka 2006 mfuko wa mawasiliano kwa wote
ulianzishwa kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa huduma za
mawasiliano katika maeneo ya vijijini na mijini.
‘Kulikuwa
na mwamko mdogo kutoka kwa makampuni ya simu katika kupeleka
mawasiliano vijijini kutokana na mazingira yake na changamoto kama
vile kuwa na idadi ndogo ya wakazi, ndio maana serikali ikaanzisha
mfuko wa upatikanaji wa huduma ya mawasiliano kwa wote ili kusaidia
katika zoezi la utekelezaji wa upanuzi wa huduma ya mawasiliano’ alisema
Mbarawa.
Hata
hivyo, Prof Mbarawa amebainisha kuwa bado mwitikio wa uombaji wa zabuni
kwa ajili ya jitihada za kupanua mawasiliano maeneo ya vijijini umekuwa
ni mdogo sana na hivyo basi kusababisha maelfu ya vijiji kukosa huduma
ya mawasiliano na hivyo kuendelea kukithiri kwa hali ya umaskini .
‘Wakati
kampuni ya simu ya Halotel ilipokuja nchini na mkakati wa kuwekeza
maeneo ya vijijini, sisi kama serikali tuliwapokea kwa mikono miwili na
tukaahidi kuwasadia baadhi ya mambo ili kurahisisha utekelezaji wa zoezi
hilo, lakini pia tukawapa masharti ya kuhakikisha wanaunganisha
mawasiliano ya mtandao kwa ofisi za vijiji 150, hospitali za umma 150,
vituo vya polisi 150, pamoja na ofisi za posta 65 na pia shule 450
‘alisema Prof Mbarawa.
Hadi
sasa, Kampuni ya simu ya Halotel kwa sasa imeunganisha huduma ya
mawasiliano kwa vijiji 1800 ambavyo vilikuwa havina huduma hiyo, na
kufikia mwishoni mwa mwaka huu kampuni ya simu ya Halotel itakuwa
imeunganisha vijiji vingine 1500 kwa mara ya kwanza ili kuhakikisha
huduma bora ya mtandao wa 3G.
‘Kampuni
ya Halotel imeunganisha zaidi ya watumiaji wa huduma ya simu 1,800,
ambao kabla walikuwa hawajaunganishwa,na muhimu zaidi, wameunganishwa
na mtandao wa kasi wa 3G kupitia fiba yenye kilomita 18,000 na hivyo
kusaidia watumiaji wa huduma hiyo kupatikana mahali popote na kwa wakati
wowote ‘ alisema Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya
Halotel, Le Van Dai.
Serikali
ya Tanzania na mshirika wake Kampuni ya Halotel wamewekeza jumla ya
dola za kimarekani billioni moja sawa na trilioni 2 za kitanzania katika
kutekelezeka upanuzi wa huduma ya mawasiliano kwa mikoa mikoa 26,
ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa kuunganisha vijiji 1,500 kupitia
mkonga wa mawasiliano unaovuka kilometa 2,500 pamoja na na kusambaza
kilometa 18,000 za fiba nchini kote, na hivyo kuifanya kampuni ya simu
ya Halotel kuwa mtandao ulionea zaidi nchini .


0 comments :
Post a Comment