Meneja
 Mawasiliano wa  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini 
(SUMATRA) bw. David Mziray  akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini 
Dar es salaam kuhusu kukamatwa kwa mabasi yaliyobainika kukiuka masharti
 ya Leseni  nyakati za asubuhi na jioni katika jiji la Dar es 
salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO bw. Frank 
Mvungi.
Baadhi
 ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano  wa  Mamlaka ya Udhibiti 
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na vyombo vya habari 
uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga kuhamasisha wadau wa Sekta
 hiyo kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta hiyo.
 (Picha na Maelezo)
……………………………………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa 
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,Kikosi
 cha Usalama Barabarani wamefanya ukaguzi katika Jiji la Dar es 
salaam,ambapo wamefanikiwa kukamata mabasi  105 na kati hayo 36 
yamefikishwa mahakamani  baada ya  kukiuka wa masharti ya leseni ya 
usafirishaji abiria.
Hayo yamwebainishwa leo  na Meneja
 Mawasiliano wa SUMATRA Bw. David Mziray wakati wa mkutano na vyombo vya
 habari uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na 
Mamlaka hiyo katika kutatua kero zinazowakabili abiria nyakati za 
asubuhi na Jioni.
Akifafanua Mziray amesema kati ya 
Machi 21-24 , 2016  ilifanya ukaguzi huo  na ili sheria iweze kuchukua 
mkondo wake Kwa wale wanaokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.
“Katika kuimarisha huduma za 
usafiri Mamlaka  imeweka utaratibu maalum wa kufanya ukaguzi katika 
maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam ikiwemo katikati ya 
jiji,Ubungo,Buguruni na Kariakoo ili kubaini wale wote wanaovunja 
sheria”.alisisistiza Mziray.
Akizungumzia baadhi ya makosa 
yalibainika kutendwa na mabasi hayo Mziray alisema kuwa ni pamoja na 
kuongeza nauli,kukata njia,kutoa huduma bila leseni ya 
usafirishaji,kutoa huduma katika njia ambazo hawakupangiwa.
Wamiliki na wafanyakazi katika 
sekta ya usafirishaji kote nchini  hasa wa mabasi ya daladala wametakiwa
 kuzingatia sheria na kanuni za usafirishaji wanapotoa huduma hiyo kwa 
umma.
Mziray  aliongeza kwamba  wananchi
 wametakiwa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale wanapobaini  basi 
walilopanda linakiuka masharti ya leseni ikiwemo kuongeza nauli,kukata 
njia,kutoa huduma bila leseni ya usafirishaji na kutoa huduma katika 
njia ambazo hawakupangiwa ambapo wananchi wanaweza kutoa taarifa kupitia
 namba za simu za bure ambazo ni 0800110019 na 0800110020.


0 comments :
Post a Comment