Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake jana Machi 27.2016 wameweza kufurahia na kumsifu Mungu kupitia huduma ya Uimbaji iliyokuwa ikitolewa katika tamasha kubwa na la Kimataifa la kumuimbia Mungu la Upendo Music Festival, lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club.
Tamasha hilo linaloandaliwa na kampuni ya Legendary Music Entertainment and Promotions Company Limited ambalo limefanyika kwa mara ya kwanza, watu mbalimbali waliojitokeza wameweza kukonga mioyo yao kwa muziki wa kusifu na kuabudu kutoka kwa wanamuziki wa injili wenye kalama na upeo mkubwa katika kusifu na kuabudu.
Baadhi ya wasanii waliokonga tamasha hilo ni pamoja na Emanuel Mbasha, Lynga George, Upendo Kihaile, Sarah Shilla, Faraja Ntaboba, Angel Magoti, Ambwene Mwasongwe na Fridah Felix.
Wengi wakiwemo Choir ya Kigogo KKKT, Gift and Beauty, Moses Saxer, Mise Ricprdias, The Joshua Generation, Glorious Worship Team, Uinjilist Choir Kimara, Doxers Praise Team, Calvary Band, The Jordan, The Next level, Chang’ombe Vijana Choir, Uinjilist Kijitonyaama, Tumaini Shangilieni Choir na wengineo.
Mwimbaji wa Injili, Angel Magoti akiimba katika jukwaa hilo la Upendo Music Festival 2016, usiku wa jana
Emmanuel Mbasha akiimba jukwaa la Upendo Music Festival 2016
Waimbaji wa muziki wa kundi la Edo na Edo..
Kundi la muziki wa injili Edo na Edo wakipata pichaa ya pamoja na baadhi ya wanumiziki wenzao wa nyimbo za Injili kabla ya kupanda jukwaa la Upendo Music Festival 2016
Mtendaji Mkuu wa Legendary Music, Amalido (kushoto) akiwa na mwanamuziki wa Injili, Emmanuel Mbasha
0 comments :
Post a Comment