Baada ya jana Jumapili kutolewa kwa taarifa ya kutokuwapo kwa mchezo wa kutafuta nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa la Afrika, kati ya Tanzania na Chad baada ya Shirikisho la Soka la Chad kutuma barua ya kujitoa katika mashindano hayo, TFF imetoa taarifa kuhusu waliokuwa wamenunua tiketi za mchezo huo ulikuwa ufanyike leo Jumatatu.
Kupitia akaunti ya twitter ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametoa taarifa kuwa waliokuwa wamenunua tiketi watarudishiwa pesa zao kuanzia kesho katika vituo ambavyo walinunulia tiketi.
Malinzi aliandika “Kufuatia mechi ya Chad kutokufanyika utaratibu unafanyika ili kesho watazamaji walionunua tiketi warudishiwe fedha zao.”
Tweet nyingine Rais huyo wa TFF aliandika “Watazamaji walionunua tiketi za mechi ya Chad watarudishiwa fedha zao kesho kwenye vituo walikonunulia tiketi jana.Waje na tiketi hizo.”