Nkupamah media:
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro akifungua mkutano huo
Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA),
Dk. Lorna Carneiro akisalimiana na Mkuu wa Huduma za Afya Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dr. Ahadiel Senkoro kabla ya kuanza kwa
Maadhimisho hayo
Wadau wakifatilia kwa makini wakati alipokuwa akiongea Rais huyo
Mkuu wa Huduma za Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dr.
Ahadiel Senkoro kabla ya kuanza kwa Maadhimisho hayo akisalimia
Mkuu
wa Idara ya Meno, Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk, Rachel Mhavile
akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam,
kuhusu maandalizi ya Maadhimisho ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani
yatakayofanyika mkoani Morogoro Machi 20,mwaka huu.kushoto ni Rais wa
Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna
Carneiro na Makamu wake, Dk. Ambege Mwakatobe.
NA KHAMISI MUSSA
CHAMA
cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), kinatarajia
kufanya matembezi katika shule mbalimbali za watoto wenye mahitaji
maalum zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro ikiwa ni katika
kuadhimisha siku ya kinywa na meno.Hayo yalisemwa na Rais wa TDA, Dk.
Lorna Carneiro, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam ambapo alibainisha kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni 'afya njema ya
kinywa ni afya ya mwili mzima'.Dk. Carneiro, alisema Machi 14 hadi 19
madaktari watatembelea shule ya mahitaji maalum ya Mtoni Maalum, Sinza
Maalum, Buguruni Maalum na zingine za Mkoa wa Morogoro ambapo pia
watafanya uchunguzi na matibabu.Alisema katika siku ya
kilele TDA itatoa huduma ya uchunguzi wa kinywa na meno kulingana
na mahitaji katika Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege ambapo mgeni rasimi
atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Rais huyo alisema pia chama hicho
kitatoa elimu, uchunguzi na matibabu ya kinywa na meno kwa waototo wenye
ulemavu wa ngozi walioko Buhangija Shinyanga.


0 comments :
Post a Comment