Chama
cha Watoa Huduma za Mitandao ya Intaneti nchini kupitia mradi wa
Tanzania Internet Exchange (TIX) imezindua mfumo mpya wa huduma ya
intaneti ya kampuni ya Akamai ambao utawawezesha watumiaji wa intaneti
nchini kupata huduma kwa uharaka zaidi.
Akizungumzia
huduma hiyo, Meneja Mradi wa TIX, Frank Habicht alisema kupita huduma
hiyo watumaji wa intaneti nchini wataweza kuperuzi katika mtandao kwa
spidi zaidi kutokana na kasi ya mawasiliano ya intaneti inayopatikana
katika mfumo huo wa Akamai.
Alisema
wameamua kutumia huduma kutoka Akamai kutokana na ubora wa huduma
zinazopatikana katika kampuni hiyo na pia wana mitambo ya kutolea huduma
katika maeneo mengi duniani.
“Kupitia
huduma hii wateja watatumia intaneti kwa gharama nafuu na hivyo itaweza
kuboresha upatikanaji wa intaneti kwa watumiaji wa Tanzania na ni nzuri
sababu inauwezo wa kuunganisha watu wengi kwa wakati mmoja na wakapata
huduma iliyo nzuri,” alisema Habicht.
Kwa
upande wa mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa amewashukuru TISPA kwa kutimiza ahadi waliyoitoa
mwaka jana ya kuongeza jitihada ili kupata huduma nyingi zaidi za mifumo
ya intaneti ili kurahisisha gharama za intaneti nchini.
Alisema
serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali ili kuboresha sekta hiyo na
kama kunakuwepo na watu wanaowapa sapoti ili kuboresha huduma ya
intaneti ni jambo la kupendeza.
“Nimefurahi
kuwepo hapa mwaka jana nilikuja na mwaka huu nimekuja tena kwa ajili ya
uzinduzi wa huduma ya intaneti ambayo itarahisisha huduma ya intaneti,
hongereni sana,” alisema Prof. Mbarawa.
Aidha
waziri amewataka TISPA kufanya jitihada zaidi ili ikiwezekana mwakani
waweze kuzindua mfumo mwingine wa huduma kutoka Limelight na Amazon.
Nae
Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary alisema wamekuwa wakifanya jitihada
mbalimbali ili kuboresha huduma ya intaneti nchini na wataendelea kuwa
mstari wa mbele katika kuanzisha huduma bora za intaneti na bora,


0 comments :
Post a Comment