Welby ahimiza maridhiano Burundi

  • Nkupamah media:
Image captionAskofu wa Justin Welby
Askofu mkuu wa Canterbury Justin Welby amemaliza ziara yake nchini Burundi na kufanikiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa Taifa hilo Pierre Nkurunziza.
Mzungumzo hayo yameangazia umhimu wa kuwepo mazungumzo ya pamoja ili kuepusha mauaji yanayoendelea kufuatia vurugu zilizozuka kutokana na uamuazi wa Rais wa taifa hilo kuwania mhula mwingine wa Uongozi.
Mamia ya watu wameuawa kutokana na vurugu hizo huku maelfu wakilazimika kuikimbia nchi yao na kukimbilia nchi jirani.
Rais Pierre Nkurunziza Katika mazungumzo hayo na kiongozi huyu wa Kiroho,muda mwingi alionekana ni mwenye furaha na tabasamu mbele ya ambapo undani wa mazungumzo hayo ilikuwa ni kuhimiza ushiriki wa pande zote ili kuhakikisha kuwa amani ya kweli inafikiwa nchini humo.
Askofu Just Welby amesema kuwa suala la maridhiano nchini Burundi linahitaji watu kujitoa muhanga.
Hata hivyo amesisitiza hatua za msingi za kuzingatiwa ili kuweza kufikiwa kwa amani ya kweli nchini Burundi.
Taifa la Burundi lililopata Uhuru wake 1962 na kupitia katika vipindi mbalimbali vya machafuko limejikuta katika upotevu wa hali ya amani katika kipindi kingine kufuatia uamuzi wa Rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza kuamua kuwania muhula mwingine hatua inayopingwa na upinzani nchini humo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment