Michezo ya mwisho ya hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA imechezwa usiku wa Jumatano na kushuhudiwa mabingwa watetezi wa kombe hilo, Barcelona wakitolewa nje ya mashindano hayo na Atletico Madrid.
Ikumbukwe mchezo wa kwanza uliochezwa katika uwanja wa  Camp Nou, Barcelona waliibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja na katika mchezo wa juzi wa marudiano Barcelona walipokea kipigo cha goli mbili kwa bila kutoka kwa Atletico Madrid.
Magoli ya Atletico Madrid yote mawili yalifungwa na Antoine Griezmann katika dakika ya 36 na 88 ya mchezo huo na hivyo kuiwezesha timu yake kufuzu hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa 3-2.
Mchezo mwingine wa nusu fainali uliochezwa juzi usiku ni Benfica iliyokuwa mwenyeji wa Bayern Munich na mchezo huo kumalizika kwa sare ya goli mbili kwa mbili.
Magoli ya Benfica yalifungwa na Raul Jimenez dk. 27 na Anderson Talisca dakika ya 76 na magoli ya Bayern Munich yakifungwa na Artulo Vidal dk. 38 na Thoams Muller katika dakika ya 52 na hivyo Bayern Munich kufuzu kwa ushindi wa goli 3-2.
Baada ya michezo ya robo fainali kumalizika, timu ambazo zimefuzu nusu fainali ni Real Madrid, Manchester City, Atletico Madrid na Bayern Munich.