Zikiwa zimesalia wiki chache kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Uingereza juzi Jumatano imetoka orodha ya wachezaji sita wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa 2015/2016 na Mchezaji Bora mwenye umri mdogo aliyecheza vyema katika msimu wa 2015/2016.
Wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa 2015/2016 ni Dimitri Payet, Harry Kane, Jamie Vardy, Mesut Ozil, N`Golo Kante na Riyad Mahrez.
Wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora mwenye umri mdogo aliyecheza vyema katika msimu wa 2015/2016 ni Harry Kane, Dele Alli, Romelu Lukaku, Ross Barkley, Jack Butland na Philippe Coutinho.