Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Bw. Anthony Mavunde, akimkabidhi, Nahodha wa NSSF, Pili
Mogola, kombe la mshindi wa kwanza wa Netiboli, wakati wa Bonanza la
Usalama na Afya mahali pa kazi, lililofanyika Dar es Salaam juzi na
kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es
Salaam juzi.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Bw. Anthony Mavunde (kulia) na Mtendaji Mkuu Mamlaka ya
Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dk. Akwilina Kayumba, wakishiriki
kufanya mazoezi na wakati wa maadhimisho ya Bonzanza la usalama na Afya
mahali pa kazi lililodhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF),Dar es Salaam juzi.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Bw. Anthony Mavunde (aliyesimama katikati), akizungumza na
wachezaji wa timu za Netiboli za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), wakati wa
Bonanza la usalama na Afya hahali pa kazi lililofanyika Dar es Salaam
juzi kwa udhamini wa NSSF.
Wachezaji
wa timu ya Netiboli ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
wakishangilia baada ya kutwaa kombe wakati wa bonanza la Usalama na Afya
mahali pa kazi, lililofanyika Dar es Salaam juzi na kudhaminiwa na
NSSF.
Mshambuliaji
wa timu ya soka ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ali
Chuo (kushoto), akimiliki mpira mbele ya mlinzi wa timu ya Wizara ya
Kazi, Abdallah Sanga, wakati wa Bonaza la Usalama na Afya mahali pa kazi
lililofanyika Dar es Salaam juzi kwa udhamini na NSSF.
0 comments :
Post a Comment