Rais Sisi na mfalme Salma wa Saudia
Mfalme wa saudia ametangaza kwamba daraja linalounganisha taifa hilo na Misri litajengwa juu ya bahari ya shamu.
Mfalme Salman alisema katika taarifa kwamba daraja hilo litaimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili.
Alitoa
tanagazo hilo wakati wa siku ya pili ya ziara yake katika mji mkuu wa
Cairo.Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi alisema kuwa daraja hilo
litatajwa baada ya mfalme huyo wa saudia.
Rais Sisi ni mshirika wa karibu wa serikali ya Saudia.
''Tulikubaliana
na ndugu yangu rais Abdul-Fattah al-Sisi tujenge daraja linalounganisha
mataifa yetu mawili'',alisema mfalme huyo.
''Hii ni
hatua ya kihistoria ya kuunganisha mabara ya Africa na Asia na
itaimarisha biashara kati ya mabara haya mawili'',aliongezea.BBC


0 comments :
Post a Comment