Waziri wa Nyumba, Ardhi na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Jiji la Dar es Salaam
litafumuliwa na kupangwa upya baada ya Ramani ya Mipango Miji (Master
Plan) mpya kukamilika.
Pia, amesema Serikali ipo kwenye mkakati wa
kuhakikisha ndani ya miaka 10 ijayo, ardhi yote nchini itakuwa
imekamilika kupimwa na kupangwa kwa matumizi mbalimbali.
Akizungumza na
wadau wa Sekta ya Uendelezaji Ujenzi Dar es Salaam jana, Waziri Lukuvi
alisema Jiji la Dar es Salaam linaongoza kwa ubovu wa upangaji miji.
Alisema kwa sababu hiyo, ameagiza kuandaliwa kwa Mpango Mji Mpya ambao
utakamilika Julai, baada ya ule wa awali kuoneakana mbovu.
0 comments :
Post a Comment