Staffan
di Mistura amesema ataitisha duru nyingine ya mazungumzo ya kutafuta
amani Syria mwezi ujao lakini amezitaka Marekani na Urusi kuhakikisha
makubaliano ya kusitisha mapigano yanazingatiwa.
Di
Mistura ameyasema hayo baada ya kuwa na kikao na Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa kuliarifu kuhusu duru ya hivi karibuni ya mazungumzo ya
kutafuta amani Syria.
Mjumbe
huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema mazungumzo hayo yalipiga hatua
licha ya kuongezeka kwa ghasia nchini Syria ambazo zinatishia kufikiwa
makubaliano ya kuvimaliza vita vya Syria.
Di
Mistura ameitaka Marekani ambayo inayaunga mkono makundi kadhaa ya waasi
nchini Syria na Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa utawala wa Rais wa
Syria Bashar al Assad kuitisha mkutano wa ngazi ya juu wa mawaziri wa
nchi zenye nguvu zaidi duniani kujadili namna ya kuheshimiwa kwa
makubaliano ya kusitisha mapigano kabla ya mazungumzo ya kutafuta amani
kuendelea.
Mapigano yamezidi Syria
Tangazo
hilo linakuja huku majeshi ya serikali ya Syria yakiishambulia hospitali
na maeneo ya makaazi ya watu katika mji wa Aleppo na kusababisha vifo
vya takriban watu 20 wakiwemo watoto wawili.
Daktari
pekee wa kuwatibu watoto katika mji huo wa Aleppo ambao unadhibitiwa na
waasi pia ameuawa katika mashambulizi hayo ya angani yaliyofanywa hapo
jana.
Katika mashambulizi mengine mashariki na magharibi mwa mji huo mapema hapo jana watu 16 waliuawa wakiwemo raia watano.
Di
Mistura amesema pande zote zilizoshiriki mazungumzo ya Geneva sasa
zanatambua haja ya kuwepo serikali ya mpito Syria ambayo itakuwa na
jukumu la kuandika katiba mpya hata kama kuna tofauti kubwa kuhusu
muundo wa serikali hiyo.
Di
Mistura ameongeza kuwa kuna uelewa mzuri kuwa kipindi cha mpito
kinapaswa kusimamiwa na serikali mpya ya kuaminika na inayojumuisha kila
upande ambayo itachukua mahala pa serikali ya sasa.
Hata
hivyo mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria amekataa kuzungumzia
suali kuu ambalo limekuwa kikwazo cha mazungumzo kusonga mbele nalo ni
hatma ya Rais Assad.
Je Assad ataachia madaraka?
Upande wa
upinzani umesiistiza kuwa Assad hawezi kuwa sehemu ya serikali mpya ya
mpito na sharti akubalie kuachia madaraka kama sehemu ya makubaliano.
Upinzani unaoungwa mkono na Saudi Arabia na nchi za magharibi,
ulijiondoa rasmi kutoka kwenye mazungumzo wiki hii ukipinga kuongezeka
kwa ghasia.
Upande wa serikali nao umesema Assad hawezi kuwa mojawapo ya ajenda ya mazungumzo ya kutafuta amani.
Hapo jana
Urusi iliutaka Umoja wa Mataifa kuliweka kundi la wapiganaji la Jaish
al Islam katika orodha ya makundi ya kigaidi kwa madai lina mafungamano
na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Dola la Kiislamu IS na
mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda.
Mazungumzo
ya kutafuta amani yamekuwa yakilenga kuvimaliza vita vya wenyewe kwa
wenyewe ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 270,000 na
kuwaaacha mamilioni ya Wasyria bila ya makaazi.(P.T)


0 comments :
Post a Comment