Mchezaji
wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu
(kulia), akiwaelekeza jinsi ya kucheza mpira wachezaji wa Timu ya vijana
waliochini ya miaka 20 ya Sunderland alipotembelea Kituo cha Michezo
cha Jakaya Kikwete Youth Park kilichopo Kidongo Chekundu Mnazi Mmoja Dar
es Salaam jana. Kanu yupo nchini kwa ziara ya siku tano kwa mwaliko wa
Kampuni ya StarTimes Tanzania ambapo jana alitoa msaada wa vyakula,
magodoro, sabuni na vyombo vya matumizi ya jikoni kwa wanafunzi wenye
mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi ya Majimatitu ya Mbagala
wilayani Temeke.
Hapa akiwa katika picha ya pamoja na timu hiyo ya watoto.
Akielekeza namna ya kucheza mpira.
Maelekezo yakiendelea.
Watoto hao wakicheza kwa kufuata maelekezo ya Kanu
(hayupo pichani)
Kanu akiwagawia fulana wachezaji hao.
Hapa akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa watoto hao.
Akiendelea kutoa maelekezo ya jinsi ya kucheza mpira.
Watoto wa kituo hicho wakimshangilia Kanu (hayupo pichani)
Kanu akiwa katika picha ya pamoja ya Buguruni Youth Centre.
Kanu akizungumza na watoto wanaopata mafunzo ya soka katika kituo hicho.
Kanu akikagua timu ya watoto hao.
Na Dotto Mwaibale
MCHEZAJI nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Nwankwo Kanu ambaye kwa sasa ni balozi
wa makampuni ya StarTimes barani Afrika ametembelea na kushiriki kwenye
mafunzo na watoto kwenye kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park cha
jijini Dar es Salaam jana.
Kanu
ambaye amekuja kwa shughuli za kampuni hiyo atakuwepo nchini Tanzania
kwa muda wa siku tano alifurahi sana kuona watoto wameandaliwa mazingira
mazuri kwa ajili ya michezo mbalimbali kwani sio wote waliopata fursa
hiyo.
“Wakati
mimi ninaanza kucheza mpira hakukuwa na kituo kizuri kama hiki wala
jezi, viatu na walimu wazuri mlio nao sasa. Hii ni fursa ya kipekee
kwenu nyinyi kuweza kuonyesha juhudi za kujifunza ili mje kuwa kama mimi siku za mbeleni.
"Leo
mimi nimekuwa maarufu ni kwa sababu nilikuwa na nidhamu, bidii, dhamira
na kuwasikiliza walimu wangu walipokuwa wananifundisha. Hatimaye leo
hii nina mafanikio makubwa, ninaishi maisha mazuri, wazazi wangu pia
wanaishi mahali pazuri, wanasafiri na kupata wanachokitaka kwa sababu tu
ya mimi kufanikiwa.” Kanu aliwaambia watoto wa kituo cha Jakaya Kikwete
Kampuni ya StarTimes ambayo imo zaidi ya nchi kumi barani Afrika
imemtua mchezaji huyo kama balozi katika
kuwawakilisha katika shughuli mbalimbali.
Kanu
anatarajia kuwa chachu kwa katika kampuni hiyo hususani katika kuboresha
na kuongeza vipindi na chaneli za michezo kwani waafrika wengi
wanapenda soka.
“Ninaamini
mchezo wa soka ndio unaopendwa na watu wengi zaidi duniani na waafrika
ni miongoni mwao. StarTimes mpaka sasa wamepiga hatua kubwa katika
kulisimamia hili, mpaka sasa tayari wana haki miliki za kuonyesha ligi
za Budensiliga na Serie A za Ujerumani na Italia.
Hiyo ni hatua kubwa kwani wateja wanafurahia michezo hiyo inyoonekana moja kwa moja kwa
vifurusushi vya bei nafuu. Kama balozi ninaahidi kushirikiana na
kampuni katika kuboresha zaidi vipindi vyake na pia kuishauri kujikita
zaidi na michezo ya nyumbani.
Kama
mnavyoona kwa mara ya kwanza tumedhamini ligi daraja la kwanza.”
Aliongezea mchezaji Kanu alihitimisha kwa kuwataka watoto wa kituoni
hapo kuonyesha bidii, utii na dhamira ya dhati kwa kila wanachokifanya,
“Ningependa kuwashauri wadogo zangu kuwa popote utakapokwenda duniani
kwenye mchezo wa soka, viwanja na mipira inayotumika ni hii hii wala
hakuna tofauti yoyote.
Hivyo
basi sioni kama kuna kitu cha kuwazuia na nyinyi msifanikiwe. Kama
nilivyowaambia awali, bidii, nidhamu, dhamira na utii kwa walimu wenu
ndio msingi wa mafanikio ya mwanasoka yeyote Yule duniani. Nawatakia
kila la kheri na siku nyingine nikija Tanzania naahidi kuwatembelea
tena.”
Kwa
upande wake Kocha Mkuu wa Kituo cha Vijana cha Jakaya Mrisho Kikwete,
Eduard Tamayo alielezea furaha yake kwa kampuni ya StarTimes kuandaa
kitu kama hiko na kukiteua kituo hiko kuwa mwenyeji wa ugeni wa Kanu
nchini Tanzania.
“Nimefurahi
sana kwa ujio aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Naijeria na vilabu
vikubwa barani Ulaya kama vile Ajax, Inter Milan na Arsena, Nwankwo
Kanu kutembelea hapa na kushiriki mafunzo na watoto. Hii ni bahati kubwa
sana kwa watoto hawa kwani ni nadra sana kutokea, kupata mafunzo,
kuzungumza, kupata ushauri na kuuliza maswali moja kwa moja kwa Kanu.
Ninatumaini itakuwa imewapa motisha kubwa sana.” Alisema Tamayo
Kocha
Mkuu huyo kituoni hapo alihitimisha kwa kuwataka wazazi kuwapeleka na
kuwasajili watoto kituoni hapo kwa mafunzo kwani wanapokelewa na
kuwapatia mafunzo mazuri kwa kuviendeleza vipaji vyao. Na kwamba kituo
hiko ni fursa kwa watanzania hivyo ni vema kukitumia vizuri.


0 comments :
Post a Comment