- Uhamisho huo utamfanya Mendy kuwa beki ghali zaidi duniani kwa sasa.
- Nyota huyo wa Monaco amesafiri kwenda Los Angeles kwa lengo la kukamilisha uhamisho huo baada ya klabu hizo mbili kukubaliana kuhusu ada ya uhamisho.
- London, England. Manchester City imethibisha kukamilisha uhamisho wa pauni 51.6milioni wa beki Benjamin Mendy kutoka Monaco.
Uhamisho huo utamfanya Mendy kuwa beki ghali zaidi duniani kwa sasa.
Nyota huyo wa Monaco amesafiri kwenda Los Angeles kwa lengo la kukamilisha uhamisho huo baada ya klabu hizo mbili kukubaliana kuhusu ada ya uhamisho.
Mchezaji huyo anamfanya kocha Pep Guardiola kutumia pauni 213.6milioni kwa msimu huu pekee, huku akiwatupia virago mabeki wake Pablo Zabaleta na Gael Clichy.
Man City tayari imewasajili Bernardo Silva, Ederson, Kyle Walker na Danilo katika lengo lake la kuhakikisha msimu huu anatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England pamoja na Ligi ya Mabingwa.


0 comments :
Post a Comment