Mwenyekiti wa zamani CHADEMA Mwanza, Adrian Tizeba ahamia CCM



Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha Demokrsaia  na Maendeleo Chedema mkoa wa Mwanza Andrian Tizeba, leo amejiunga rasmi na CCM wilayani  Sengerema tawi la Lugata.

Tizeba ambaye alitangaza kujivua uanachama wa chadema Machi 29 mwaka huu baada ya kusimamishwa uongozi kwa muda wa mwaka mmoja, na kutangaza kuachana na siasa, amekabidhiwa kadi hiyo  na katibu wa tawi hilo Alfred Mwambala.

Akizungumza kwa njia ya simu, Tizeba amesema uamuzi wake si wa kulazimishwa na mtu bali, ameona ni vema arudi kwenye chama chake cha awali.

Tizeba ambaye ni kaka wa mbunge wa jimbo la Buchosa, Charles Tizeba amesema, nia na dhumuni la kujiunga na chama hicho ni kutokana na utendaji wa Rais John Magufuli anaoufanya
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment