Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amefanya ziara mkoani Kagera ikiwa ni moja ya ziara anazozifanya kwa siku za karibuni kutembelea mikoa mbalimbali kuona utendaji kazi wa maeneo yanayohusu wizara yake pamoja na kuwapatia vitendea kazi watumishi wa maeneo hayo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na uongozi wa mkoa wa Kagera baada ya kuwasili mkoani hapo akiwa kwenye ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mkoa huo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili mkoani Kagera kwa ajili ya kufanya ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mkoa huo. Wengine pichani ni Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw,Jackson Msome na Kaimu katibu tawala mkoa wa Kagera, Bw.Adam Mohamed Swai.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akikabidhi Tablet tano kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maafisa habari wa mkoa wa Kagera. Bwana Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw. Jackson Msome ambaye anamwakilisha Mkuu wa mkoa wa kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati wa ziara ya waziri huyo katika mkoa wa Kagera.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akizungumza jambo na waandishi wa habari wakati alipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Kaitaba. Uwanja huo umeshawekwa nyasi za bandia na maboresho mengine yanaendelea.
0 comments :
Post a Comment