Umoja
wa Asasi za Vijana mbalimbali wamekutana Jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki katika kujadili kwa kina na kutoa maoni yao kuelekea Bunge la
bajeti pamoja na mustakabali mzima wa vijana hapa nchini hasa katika
mambo yanayoleta tija na changamoto wanazokumbana nazo katika masuala ya
ajira.
Katika
mkutano huo, Mbunge wa Viti Maalum, ambaye anawakilisha Vijaana Bungeni
kutokea Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Zainabu Katimba alikuwa mgeni
rasmi na amepokea maoni ya Vijana hao kwa ajili ya kwenda kuyasemea
Bungeni katika kikao cha bunge kijacho.
Aidha,
Mkutano huo ulioandaliwa na Asasi ya Vijana ya (Tanzania Young Vision
Association-TYVA), huku ikiziusisha asasi Zaidi ya tisa za vijana
zikipata kushiriki katika mkutano huo.
Mbunge anayewakilisha Vijana Bungeni, Mh. Zainabu Katimba akitoa maoni yake juu ya vijana


0 comments :
Post a Comment