Baada
ya suala la rushwa hasa kwa watumishi wa Serikali kuendelea kuwa kubwa,
Mkuu wa Mkoaa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda ametangaza ofa kwa
wakazi wa jiji hilo muda na wakati wowote kujitokeza katika ofisi yake
kuchukua kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kulipia endapo Mwananchi
ameombwa rushwa na watumishi hao wa Serikali.
RC
Makonda amebainisha kuwa kutokana na suala la watumishi hasa wa kada ya
Afya kuwadai wananchi rushwa pamoja na maafisa wengine katika jiji la
Dar es Salaam, amekuja na Mkakati huo wa kutoa fedha kwa kiasi chochote
kile ambacho Mwananchi atakiitaji endapo ataombwa rushwa na mtumishi wa
Serikali ndani ya Mkoa wake.
Aidha,
Makondna pia amewataaka wananchi kuzingatia sheria na kanuni mbalimbali
zilizowekwa bila kuvunja sheria na kubainisha kuwa, yeye na timu yake
wataendelea kutatua kero zinazowakabili wananchi popote pale walipo
ndani ya Jiji.
Kwa
upande wa watu wanaofanya shughuli za kuombaomba barabarani, RC Makonda
amewataka wananchi kusitisha hatua ya kuwapatia pesa watu hao pamoja na
watoto wao kwani wengi wao wamegeza suala hilo kama mtaji na kwa sasa
wanandaa utaratibu maalum wa kuweza kuwaondoa kwenye maeneo yote ya
Jiji.
Makonda
ameongea hayo hivi karibuni kupitia kipindi cha televisheni ya Chaneli
ten, katika mada maalum juu ya Kukusanya kero kwa wakazi wa Dar es
Salaam na kupokea kero mbalimbali ambazo aliwahidi wananchi waliotoa
maoni yao kuwa atazifanyoa kazi yeye pamoja na timu yake huku baadhi ya
kero zingine akizitolea ufafanuzi papo hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
0 comments :
Post a Comment