Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka (Kulia)
akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati
wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Mjumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Dkt. Anaclet Kashuriza (Aliyesimama)
akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati
wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Baadhi
ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
wakifurahia jambo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na
viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya
TADB.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi (Kulia) akizungumza mbele ya
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja
kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
na menejimenti ya TADB.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Mary Nagu
(Katikati) akifuatilia maelezo yaMkurugenzi Mwendeshaji wa TADB (hayupo
pichani) wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi
kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Baadhi
ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
wakitoa michango yao wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na
viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya
TADB.
Baadhi
ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
wakitoa michango yao wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na
viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya
TADB.
Baadhi
ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
wakitoa michango yao wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na
viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya
TADB.
Wabunge
wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji imeipongeza
Serikali kwa kuanzisha kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
yenye lengo la Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula
ambao ni endelevu nchini Tanzania na kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya
Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia
kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
Wakizungumza
na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya
TADB wakati wa vikao vya kamati za Bunge vinavyoendelea jijini Dar es
Salaam. Wabunge hao wamesema kuwa TADB imekuja wakati muafaka kwa kuwa
itachagiza juhudi za kuinua na ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini
nchini Tanzania.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Mary Nagu amesema kuwa licha ya umuhimu wa
Sekta ya Kilimo, bado ukuaji wa sekta hiyo ulikuwa ukikabiliwa na
changamoto mbali mbali kuu ikiwa ni Ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa
fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini.
“Kwa
kweli tunapongeza kwa kuanzishwa Benki hii kwa kuwa kwa miaka mingi
mikopo mingi kutoka taasisi za fedha imekuwa ikielekezwa zaidi kwenye
upande wa biashara za bidhaa na kuwa na riba kubwa kwenye mikopo ya
kilimo,” alisema Mhe. Nagu.
Wabunge hao wametoa wito kwa Serikali kuiongezea mtaji Bnki hiyo ili kuongeza kasi ya utendaji kazi wa Benki hiyo.
Akizungumza
kwenye kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi,
Dkt. Florens Turuka alisema kuwa TADB inajihusisha na aina zote za
kilimo kwa ule wigo mpana wa maana ya kilimo, ambao inahusisha mazao,
ufugaji, uvuvi, na bidhaa zitokanazo na misitu. Na kuongeza kuwa katika
kusaidia minyororo ya thamani ya mazao ya kilimo, TADB itakuwa inatoa
fedha kwenye hatua mbali mbali za Uzalishaji na uongezaji wa thamani
kama vile Uzalishaji wa awali; uhifadhi; usindikaji; uchakataji;
usafirishaji; na masoko.
“Uanzishwaji
wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini kama taasisi ya maendeleo ya
fedha, kulitokana na Wizara yangu, na baadaye mawazo ya Wadau mbalimbali
chini ya uratibu wa Baraza la Taifa la Biashara kuhusu jinsi Tanzania
inavyoweza kufikia mapinduzi ya kilimo,” aliongeza Dkt. Turuka.
Kwa
mujibu wa Dkt. Turuka, katika maazimio kumi (10) ya Kilimo Kwanza
yaliyofikiwa mwaka 2009, azimio la tatu lilikuwa kuanzishwa kwa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo. Hivyo uanzishwaji wa benki hii ni muendelezo wa
Serikali katika kutimiza na kutekeleza maazimio ya “KILIMO KWANZA”. Hii
ilitokana hasa na kuwepo kwa changamoto mbali mbali kwenye Sekta ya
Kilimo ikiwemo upatikanaji wa fedha na mikopo ya riba nafuu katika
kuendeleza sekta ya kilimo nchini kwa miradi mikubwa ya kilimo, ya kati
na midogo inayolenga kuimarisha minyororo ya thamani ya Kilimo.
Naye
Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi alisema kuwa kama
yalivyo matarajio ya Serikali, kuanzishwa na kuanza kufanya kazi kwa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini, kunategemewa kuwa na umuhimu wa
kusaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda vya ndani hivyo kusukuma
ndoto ya Serikali kufikia lengo lake la Kujenga Uchumi wa Viwanda.
Ameongeza
pia TADB inatarajia kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na
vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo na mifugo
pamoja na kuboresha kwa upatikanaji wa mikopo na huduma za kifedha
kwenye miradi ya maendeleo ya Kilimo kwa riba nafuu zilizo chini ya
viwango vya kibiashara kwenye soko.
Benki
ya TADB ni mali ya Serikali kwa Asilimia 100 ya Hisa na kwa kuzingatia
muundo wa uendeshaji wa shughuli za Serikali hususan kwenye masuala ya
kifedha, Benki ya Maendeleo ya Kilimo iko chini ya Wizara ya Fedha na
Mipango. Hali kadhalika, benki iko chini ya Uangalizi wa Msajili wa
Hazina kama yalivyo mashirika mengine ya Umma. Hata hivyo,
kiutekelezaji, TADB inajihusisha moja kwa moja na Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, kwani muktadha wa uanzishwaji wake umelenga moja kwa
moja kwenye Sekta ya Kilimo kuliko Sekta nyingine yoyote.
0 comments :
Post a Comment