Baadhi
ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekishiutumu Chama cha Wananchi
(Cuf) pamoja na viongozi wao kwa kukosa uzalendo kutokana na kauli zao
za kuunga mkono wahisani kuisitishia misaada Tanzania.
Hayo
yalisemwa na Mwakilishi wa kuteuliwa kutoka katika chama cha Ada-Tadea,
Juma Ali Khatib ambaye aligombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu
wa marudio, alipokuwa akichangia hotuba ya Rais wa Zanzibar kwenye
baraza hilo mjini hapa.
Alisema,
viongozi wa Cuf wameonesha udhaifu mkubwa wa kukosa uzalendo kwa
kitendo chao cha kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo kususa misaada
kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema,
Zanzibar ni nchi yenye kufuata katiba yake kwa hiyo ilikuwa na mamlaka
kamili kupitia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kuitisha uchaguzi wa
marudio baada ya kuufuta wa Oktoba 25, mwaka jana.
“Nimesikitishwa
na kauli za viongozi wa Cuf kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo
kuhusu uamuzi wa kususia misaada kwa Tanzania. Viongozi hao wameonesha
udhaifu na kukosa uzalendo,” alisema Khatib.
Alisema
chama chake kiliamua kuingia katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20 kwa
sababu umeitishwa na chombo halali kwa mujibu wa katiba, chenye
majukumu ya kusimamia uchaguzi kikiwa hakiingiliwi na mtu yeyote.
Mwakilishi
wa Jimbo la Mfenesini , Machano Othman Said, alisema kitendo cha
viongozi wa Cuf kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo kususa kutoa
misaada kwa Tanzania hakikubaliki hata kidogo kikionesha udhaifu mkubwa
wa viongozi hao katika uzalendo wa nchi.
0 comments :
Post a Comment