WANANCHI WA KATA YA MANG'OLA WALALAMIKIA KITENDO CHA MKUU WA WILAYA KUFUNGA SHUGHULI ZA UVUVI ZINAZOFANYWA NDANI YA ZIWA EYASI


 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Mang'ola hiii leo wakati alipofanya ziara katika kata hiyo iliopo ndani ya wilaya ya karatu mkoani Arusha
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anajaza mchanga kwa ajili ya kufetua matofali   hiii ikiwa nimoja ya mradi ambao ameutembelea katika kata hiyo
 Diwani wakata ya mang'ola  Lazaro Gege  akiwa anampa maelezo kwa ufupi  ya mradi wa matofali kaimu katibu mkuu wa vijana CCM taifa


Mwenyekiti wa umoja wa  vijana wa ccm Mkoa Arusha Sabaya Lengai akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Mang'ola hii leo wakati wa ziara ya kaimu katibu mkuu wa vijana taifa
baadhi ya wananchi wakiwa wanaendelea kufatilia mkutano huo
Na Woinde Shizza,Karatu

Wananchi wa kijiji cha Malekichanda kilichopo katika kata ya Mang’ola  wilayani karatu mkoani Arusha wamelalamikia kitendo cha serekali kufungia ziwa  Eyasi na  kusema kuwa kitendo hicho kimewafanya vijana wengi kukosa kazi na kinaweza kusababisha wananchi wa eneo hilo kukumbwa na baa la njaa kutokana na kumaliza chakula  chote ambacho walikuwa wamekihifadhii kwa ajili ya chakula  cha akiba akiba.

Hayo waliyasema leo wakati   Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alipofanya ziara yakutembela na kukagua baadhi ya miradi inayofanywa na  chama pamoja na kuongea na wananchi wa kata hiyo.

Walisema kuwa wanasikitishwa sana na kitendo cha  mkuu wa wawilaya  kuwasimamisha  shughuli zao za uvuvi kwani ndizo walizokuwa wakizitegemea  katika kujipatia kipato pamoja na chakula katika kijiji hicho na kata kwa ujumla.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Kristopher Nyato alisema kuwa tangu marchi 19 walizuiwakufanya shughuli zao za uvuvi katika eneo hilo na kupewa masaa 24 kuondoka katika eneo hilo kwakile kilichodaiwa kuwa eneo hilo limekubwa na ugonjwa wa kipindu pindu.

“unajua  mimi  ni mfanya biashara nimetokea mbali nasio mimi tu tupo wengi naninavijana wangu ambao nimekuja nao hapa kwa ajili ya shughuli hii ya uvuvi sasa  tarehe hiyo  19 mwezi wa tatu mkuu wawilaya alikuja apa na askari nakutupa masaa 24 tuwe tumeondoka kuhoji nini ni wakatuambia  ni pachafu  mara waseme kuna kipindu pindu tukawaambia kama ni pachafu watuache wakagoma wakasema tumesema muondoke ndiposisi  kwa kuwa tunaogopa nakamaunavyojua wananchi tulivyo waoga tukaondoka na tulivyoondoka walituambia  baada ya siku chache wangefungua lakini adi sasa apajafunguliwa  tunateseka sana ata vyakula vyetu vya akiba tumemaliza yaani apa ni tabu tu”alisema Nyato

Kwa upande wa mwananchi mwingine aliejitambulisha kwa jina la Wiliam Jonas alisema kuwa mara baada ya ziwa hilo kufungwa wamekuwa wanaishi maisha ya kuomba omba ,wao kama wananchi wanagawana chakula walichokuwa wamekiifadhi na kinakaribia kwisha na vijana wengi walikuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika ziwa hilo wamekuwa wazururaji.

Akiongea na wananchi hao Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alisema kuwa   yeye kama katibu amesikia malalamiko yao naatayafanyia kazi kwa kukutana na mkuu wawilaya nakuona ni jinsi gani ambavyo wataweza kutatua tatizo hilo.

Gazeti hili halikuishia hapo ilibidi kumtafuta mkuu wa wilaya ya karatu Omary Kwaanq ili kuzungumzia tuhuma hizi nakusema kuwa kweli wamelifunga ziwa hilo kutokana na ugonjwa wa kipindu pindu ambao umeikumba wilaya yake .

Alisema kuwa mpaka sasa wilaya yake ina wagonjwa 70 wa kipindu pindu na wamefanya utafiti ukaonyesha wagonjwa wengi wametokea maeneo ya ziwa hilo.

“tumefanya utafiti kiukweli kwa kushirikina na mtaalamu wamagonjwa wa milipuko nakubaini kuwa maji yale ya ziwa yana chembe chembe za wadudu wanao eneza ugonjwa wa kipindu pindu hivyo tukaamua ni borakufunga ziwa ilo ili wananchi wasiendelee kuzurika na ugonjwa huo.

Aliongeza kuwa mara baada ya kuona maji yale ya ule mto yana vimelea vya ugonjwa wa kipindu pindu ndio maana wakaona ni bora wafunge ziwalile  ili wananchi wasiendele kupata ugonjwa huo hatari.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment