Michezo ya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea usiku wa Jumatano kwa michezo miwili, Wolfsburg wakiwa wenyeji wa Real Madrid na PSG ikiwakaribisha Manchester City.
Matokeo ya michezo hiyo Wolfsburg iliibuka na ushindi wa goli mbili kwa bila dhidi ya Real Madrid, magoli yakifungwa na Ricardo Rodriguez dk. 18 na Maximilian Arnold dakika ya 25.
Mchezo mwingine PSG ilitoka sare ya magoli mawili kwa mawili, magoli PSG yakifungwa na Zlatan Ibrahimovic dk. 49 na Adrien Rabiot na dakika ya 59 na magoli ya Manchester City yakifungwa na Kevin De Bruyne dk. 38 na Fernandinho dk. 72.