Hatimaye baada ya safari ndefu ya Ligi ya Uingreza msimu wa 2015/2016, Leicester City imekuwa bingwa wa ligi hiyo kipenzi cha watu wengi duniani baada ya sare ya goli 2-2 ya jana usiku ya kati ya Chelsea na Tottenham.
Leicester City imetwaa huo kwa kuwa na alama 77 ambazo haziwezi kufikiwa na Tottenham inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 70 na ikiwa imesalia michezo miwili kwa kila timu kumaliza michezo iliyosalia.
Ubingwa huo umekuja baada ya sare ya goli 2-2 Chelsea na Tottenham katika mchezo wa jana usiku ambapo Tottenham ilikuwa ya kwanza kufungwa kupitia Harry Kane dk. 35 na Son Heung-min dk. 44 na Chelseea kusawazisha kupitia Gary Cahill dk. 58 na Eden Hazard katika dakika ya 83