Kauli
mbiu ya Maadhimisho haya mwaka huu ni “Kupata Taarifa ni Haki yako ya
Msingi, Idai’. Maadhimisho haya yanafanyika kitaifa kwa mara ya nne na
yanalenga kukumbusha Umma na dunia kwa ujumla umuhimu wa vyombo vya
habari kufanya kazi yake bila kuingiliwa na mtu ama chombo chochote.
Bi.Valerie
Msoka kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA),
akiongoza kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
kwa mwaka 2016 yanayofanyika kitaifa katika hoteli ya ufukweni ya
Malaika Jijini Mwanza.
Zaidi ya wadau 250 wakihusisha
waandishi wa habari wakongwe na wapya, wahariri, viongozi wa mashirika
wahisani (ya kimataifa na ya hapa nchini) wawakilishi wa mihili ya nchi,
wasomi wa vyuo vikuu na balozi mbalimbali wamekusanyika jijini hapa kwa
maadhimisho hayo ambayo kilele chake ni kesho.
Watoa
Mada katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari 2016 yanayofanyika Jijini Mwanza. Kilele cha Maadhimisho hayo
kinafanyika kesho Mei 3,2016 ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman. Pia Waziri wa Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Nhaute pamoja na wageni wengine
waalikwa wanatarajia kuhudhuria maadhimisho hayo.

Usia
Nkhoma Ledama ambae ni Afisa Habari kutoka UN Information Centre
(Tanzania) akiwasilisha Mada katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
Wanahabari
na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
0 comments :
Post a Comment