Hatimaye tetesi zilizokuwa zikisikika kwa muda mrefu sasa zimekamilika za kocha wa zamani wa vilabu vya Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid, Jose Mourinho kujiunga na Manchester United baada ya kusaini mkataba wa miaka minne kuionoa klabu hiyo ambayo kwa miaka ya karibuni imeonekana kuyumba na kushindwa kuonyesha kiwango ambacho kilikuwa kimezoeleka.
Mourinho amesaini mkataba ambao uamwezesha kupokea kitika cha Pauni Milioni 15 kwa mwaka na katika mkataba huo wa miaka mine kuna kipengele ambacho kinawezesha mkataba huo kuvunjika baada ya miaka mitatu na hakuna hatua ambayo inaweza kuchukuliwa.
Baada ya kusaini mkataba huo Mourinho alisema kuwa “Kuwa meneja wa Manchester United ni heshima kubwa, ni klabu kubwa ambayo kila mtu duniani anaitamani, ina vitu ambavyo vilabu vingine duniani hawana,” alisema Mourinho.


Blogger Comment
Facebook Comment