Nywele za Wema Sepetu kwa wiki hutumia Sh milioni 1.2


Miss Tanzania 2006, Wema Isaack Sepetu, ameweka wazi kwamba hutumia shilingi milioni 1.2 kwa ajili ya kutengeneza nywele zake kwa wiki moja.
 
Pia hutumia Sh 30,000 ya chakula kwa siku na kama atanunua na chakula cha mbwa wake huwa anatumia Sh 50,000 kwa siku.
 
Hata hivyo, Wema amesema si kila wakati hutumia kiasi hicho cha fedha, bali hutegemeana na aina ya nywele anazotengeneza.
 
Alifafanua zaidi kwamba gharama hizo pia zinatokana na kutumia ‘weaving original’ lakini wakati mwingine hutumia hadi laki moja na nusu kwa nywele za kawaida kama rasta.
 
“Huwa nabadilisha nywele kila baada ya wiki ambapo siku nyingine natumia milioni moja, siku nyingine laki saba au tano kwa sababu sipendi kukaa na nywele muda mrefu na nywele zangu ni ‘orijino’,”alisema.
 
Wema aliongeza kwamba anachopenda zaidi kwake ni kuwa na muonekano mzuri wa urembo kwa kuwa urembo upo kwenye damu yake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment