Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Asha-Rose Migiro akizundua Kamati itakayoshughulikia changamoto za
usalama za watu wenye Ualbino nchini kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hii imeundwa kutokana na ahadi ya
Rais Jakaya Kikwete aliitoa wakati alipokutana na viongozi wa Chama cha
Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es
Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Haji Janabi, na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Ernest Mangu.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akiwafafanulia
jambo wajumbe wa Kamati
itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini.
Kamati hiyo ambayo ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa alipokutana
na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu,
imezinduliwa leo na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro
(katikati meza kuu) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza
kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
Mwenyekiti wa Chama cha Albino
nchini (TAS), Ernest Kimaya akimshukuru Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (hayupo pichani), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP
Ernest Mangu (kulia meza kuu), kwa msaada wao ambao umesaidia matukio ya
utekaji na mauaji ya albino kupungua kwa kiasi kikubwa. Pia alisema
Kamati iliyozinduliwa itaongeza nguvu zaidi katika kukabiliana na
changamoto ambazo zinawakabili za usalama wao nchini. Kushoto meza kuu
ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi.
Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Dk. Migiro kwa niaba ya Waziri
Chikawe, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Asha-Rose Migiro akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Haji Janabi (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Ernest Mangu mara baada ya kupokelewa Waziri huyo katika ofisi za
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili azindue Kamati itakayoshughulikia
changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini, kwa niaba ya Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hiyo imeundwa
kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na
viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi
huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Asha-Rose Migiro (wanne kulia-mstari wa mbele), Kaimu Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati), na Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia) wakiwa katika
picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa Kamati
itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini.
Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Migiro kwa niaba ya Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Hata hivyo Kamati hiyo imeundwa
kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na
viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi
huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, jijini Dar es Salaam


0 comments :
Post a Comment