Bonanza maalum kwa ajili ya wanavyuo wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki (Mei 21, 2016) Jijini Arusha lilifana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakijiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF.
Viongozi
wa vyuo mbalimbali mkoani wakiwa katika picha ya pamoja Afisa Mfawidhi
wa PSPF Arusha Bw. Philbert Leina (wa tatu kutoka kushoto, mstari wa
nyuma) baada kikao cha maandalii kilicho fanyika katika ofisi za PSPF
mkoa wa Arusha.
Tamasha
hilo lililofanyika katika viwanja vya chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)
kilichopo Njiro jijini Arusha, lilijumuisha vyuo vya Makumira, Mt. Meru,
SAUT, MAN U (Chuo Kikuu cha Arusha), Chuo cha Ufundi Arusha na IAA.
Wanachuo wa IAA, wakishangilia baada ya timu yao kuibuka mshindi katika mpira wa miguu.
Michezo iliyoshindaniwa ni pamoja na Football, Netball, Basketball na Volleyball, hata
hivyo mchezo uliovuta hisia za washiriki wengi ni mchezo wa mpira wa
miguu ambapo timu ya Chuo cha Uhasibu Arusha kilibuka mshindi
Wanachuo wakifatilia Burudani kutoka kwa Mjomba Band
Akifungua
mashindano hayo, Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Bw. Daniel Machunda
aliwataka wanavyuo hao kutumia michezo hiyo kama sehemu ya kujenga
uhusiano Mwema na ushirikianao kati ya vyuo na kati ya yao wenyewe.
Pia
aliishukuru PSPF kwa kuandaa Bonanza hilo ambalo msingi wake mkubwa
ulikuwa ni kuwaelimisha wanavyuo juu ya huduma za PSPF. “Hili jambo
mnalofanya PSPF ni jambo zuri sana kwa wanafunzi wa vyuo vya Arusha
pamoja kutoa burudani lakini pia mnawapatia ufahamu juu ya Mfuko wenu
(PSPF), hili ni jambo zuri sana na ninawaomba wana vyuo kuazingatia
elimu mtakayopatiwa na wakati ukifika mfanye maamuzi sahihi,” alisema
Bw. Machunda.
Ukaguzi wa timu kabla ya mchezo, wa tatu kulia ni Afisa Mfawidhi wa PSPF Arusha Bw. Philbert Leina.
Kwa upande wake Afisa mchezo wa Mkoa wa Arusha, alisema
amefurahishwa sana kwa PSPF kuandaa Bonanza hilo kwa wanavyuo wa mkoa
wa Arusha na kuwataka wanavyuo kuhakikisha mashindano yanaanza na
kumalizika kwa usalama, lengo likiwa ni kudumisha upendo na uhusiano
Mwema kati ya vyuo hivyo.
Wawakilishi
wa vyuo vilivyoibuka washindi katika bonanza hilo wakiwa na katika
picha pamoja na Mgeni rasmi baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
Kwa
upande wake, Mwakilishi wa mkuu wa Chuo cha Uhuasibu Arusha, Bibi. Laura
Kishala Aliishukuru PSPF kwa kuweza kuanda Bonaza hilo kwa vyuo vya
Arusha, akifafanua zaidi alisema, “Bonanza hili mliloliandaa hakika ni
jambo zuri sana kwa wanafunzi wetu kwani michezo ni afya, na pia
tunashukuru kwa elimu juu ya Mfuko wa PSPF, nina imani sasa wanafunzi
wetu wamepata elimu ya kutosha juu ya PSPF, “.
Pamoja
na mashindano hayo, pia wanavyuo hao walipata burudani kutoka kwa
balozi wa PSPF Mrisho Mpoto, ambaye alikuwa na kikundi chake cha sanaa.
Mpoto alikuwa ni burudani tosha kwa wanavyuo hao.
Baada
ya kupata elimu juu ya Mfuko, hususan katika Mpangowa uchangiaji wa
hiari (PSS), idadi kubwa ya wanavyuo hao walijiunga na mpango huo.
Wanavyuo wakijiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS)
Wanavyuo wakijiunga na Mpango wa Uchagiaji wa Hiari(PSS)
“Hawa
jamaa (PSPF) wapo vizuri sana, kwani wametupatia burdani na elimu ya
kutosha juu ya PSPF, hakika sasa nimepata uelewa wa kutosha juu yao na
ukifika wakati wa kuchagua Mfuko nitafanya maamuzi sahihi,” alisikika
mmoja wa wanavyuo hao.
Blogger Comment
Facebook Comment