Siku kadhaa baada ya kumfukuza aliyekuwa kocha wake Louis Van Gaal, Manchester United leo imetoka taarifa kuwa kocha Jose Mourinho amejiunga na Man United baada ya kukutana na uongozi wa klabu hiyo na kusainishwa mkataba ambao utamfanya kuanzia sasa kuwa kocha wa klabu hiyo.
Mtandao wa Skysports umeripoti kuwa Mourinho alikutana na viongozi wa Man United leo mchana katika hoteli iliyopo katikati ya jiji la London ambapo moja ya viongozi aliokutana nao ni Mkurugenzi Mkuu wa Man United, Ed Woodward.
Taarifa zimeeleza kuwa Mourinho alikaa katika hoteli hiyo kwa saa moja na dakika 30 na baada ya hapo alionekana akitoka akiwa na hati mbalimbali pamoja na chumba ya mvinyo ambapo aliingia kwenye gari iliyompeleka eneo hilo na kisha kuondoka.
34A5283700000578-3611017-image-a-22_1464278272838
Mourinho akiondoka hotelini.
Aidha baada ya muda mfupi, beki wa zamani wa Man United, Rio Ferdinand aliandika ujumbe kuwa Mourinho amesaini mkataba na Man United.