Bingwa wa zamani wa mchezo wa Masumbwi Dunia kwa uzito wa juu (World Heavyweight Champion) aliyeaminika kuwa mmoja kati ya Mabondia bora zaidi kuwahi kutokea, Muhammad Ali maarufu kama “The Greatest” amefariki Dunia mapema leo katika hospitali ya Phoenix-area iliyopo Phoenix, Arizona alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Muhammad Ali ambaye alikuwa ni Bingwa mara tatu wa ngumi za Uzani wa Juu Duniani, amefariki akiwa na umri wa Miaka 74.
Muhammad Ali aliyestaafu ndondi za kulipwa mwaka 1981 aligundulika kuwa na ugojwa wa Parkinson (Parkinsons Disease) Mwaka 1984 na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo hadi alipopatwa na mauti.
Mbali na ugonjwa huo pia Ali alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi pamoja na maambukizi katika njia ya mkojo.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. Amina
Blogger Comment
Facebook Comment