Matumaini ya Tanzania kushiriki Kombe la Mataifa Afrika mwakani yanayotaraji kufanyika nchini Gabon yamepotea baada ya kukubali kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa Mafarao wa Misri.
Katika mchezo ambao umepigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Tanzania ilionekana kuanza mchezo huo vizuri na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni kwa Misri, mashambulizi ambayo yalionekana kutokuza matunda kutokana na uimara wa walinzi wa Misri.
Misri iliandika goli la kwanza kupitia kwa Mohamed Salah katika dakika ya 43 kwa kutumia vema faulo ambayo waliipata baada ya beki wa Tanzania, Haji Mwinyi kumchezea faulo mshambuliaji wa Misri, Nagram Fahmy.
Kipindi cha pili kilianza kwa mchezo kupoa lakini katika dakika ya 58, Mohamed Salah aliiandikia Misri goli la pili nala ushindi kwa mchezo huo baada ya kuwapita mabeki wa Tanzania na kupiga mpira ulioenda moja kwa moja nyavuni.
Hata hivyo pamoja na kipigo hicho Tanzania ilipata nafasi ya kufunga goli la kufutia machozi katika dakika ya 53 baada ya kupata penati iliyopigwa na nahodha, Mbwana Samatta na kupaisha mpira huo juu.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Misri sasa imefikisha alama 10 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine na hivyo kufuzu kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2017, Nigeria ikiwa nafasi ya pili ikiwa na alama mbili na Tanzania alama moja ikishika nafasi ya tatu.
Blogger Comment
Facebook Comment