Kama ukitaja orodha ya wachezaji walio katika kiwango bora cha soka na wanaong’aa zaidi kwa sasa huwezi kuacha kumtaja staa wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya West Ham United, Dimitri Payet ambaye katika michezo ya Uefa Euro 2016 inayoendelea Ufaransa katika michezo miwili ambayo timu yake ya taifa imecheza amefunga magoli mawili na kutoa pasi ya goli moja na hivyo kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha Ufaransa.
Payet ambaye kwa klabu anakipiga West Ham kwa uwezo alioonyesha msimu wa 2015/2016 aliisaidia West Ham kuwa timu bora kwa msimu huo na yeye kuwepo katika kikosi bora cha msimu wa 2016/2017.
Kutokana na uwezo wa Payet anaoonyesha sasa katika Euro 2016, inasemekana kuwa tayari vilabu kama Real Madrid ya Hispania na Chelsea ya England zimeanza kuonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambaye hucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji.
Wakala wake Mark McKay amekaliliwa na mtandao wa Mirror akieleza kuwa mteja wake bado ana furaha kuendelea kuichezea West Ham.
“Pamoja na kumuhusisha lakini ana furaha kuwa West Ham na mengine ni kuwaachia West Ham,
“Anafanya vizuri akiwa na Ufaransa na unaweza kumuona, siyo siyo sahihi kuzungumza hilo kwa sasa lakini soka ni soka, hatuwezi jua,” alisema McKay.


Blogger Comment
Facebook Comment