Kufuatana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971, ndoa ni muungano wa hiari kati ya mwanamme na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa  maisha yao.
Aina za ndoa
Kuna aina mbili za ndoa;
  1. i) ndoa ya mke mmoja, hii ni ndoa ambapo mwanamme ana mke mmoja tu.
ii] ndoa ya wake wengi, hii ni ndoa ambayo
mwanamme ana wake zaidi ya mmoja.
Ndoa itokanayo na dhana ya ndoa; hii ni ndoa ambayo mwanamke na mwanamme wamekaa pamoja ndani ya nyumba kama mke na mme kwa muda wa miaka miwili na kuendelea na wote wakapata hadhi ya kuwa wanandoa.
Vipengele gani vya kuzingatia ili wanaotaka kufunga ndoa wakubaliwe kisheria kufunga ndoa
(a) Ni lazima muungano uwe wa hiari
Mume na mke wawe wameamua kuishi pamoja kwa ridhaa yao wenyewe. Hii inamaanisha kusiwe na kulazimishwa, kuhadaiwa kwa aina yoyote kwani
muungano kama huo utakuwa batili kisheria.
Ni kosa la jinai kushiriki katika shughuli ya ndoa ambayo mmoja wapo au wote wamelazimishwa kufunga ndoa.
(b) Muungano uwe ni kati ya mwanamke na mwanamme
Muungano wa watu wa jinsia moja hata kama ni wa hiari muungano huo hautambuliki kisheria.
Pia mtu huhesabika mwanamke au mwanamme kutokana na
sehemu za siri alizozaliwa nazo na siyo alizozipata baadaye.
Jamii inachukulia kuwa ndoa ni njia pekee
ya kujipanua, upanukaji huku ni kwa kuzaa watoto.
Kwa hali hiyo ili kupata watoto ni lazima ndoa iwe kati ya mwanamme na mwanamke.
(c) Muungano huo uwe unakusudiwa kuwa wa kudumu
Pamoja na kuwa mwanamke na mwanamme wameamua kuishi pamoja kwa hiari yao lakini siyo kwa kutodumu muungano huo hautambuliki kisheria kama ndoa.
Muungano ni lazima uwe wa kudumu
maisha yote au kama mmoja wao amefariki au kama ndoa imekumbwa na matatizo na mahakama ikaona ni bora kutoa talaka kwa yeyote aliyefika kulalamika.
(d) Wanandoa wasiwe maharimu
Maharimu ni watu walio na mahusiano ya karibu ya damu au kindugu.
Wawili wanaoamua kufunga ndoa wasiwe na uhusiano wa karibu kindugu.
Inakatazwa katika kifungu cha 14 cha Sheria ya ndoa ya mwaka
1971 mtu kuoa au kuolewa na mzazi wake, mtoto au mjukuu wake, kama ni dada yake, mama au shangazi au baba wa mjomba wake, baba au mama wa kambo na mwanaye aliyemfanya kuwa mtoto
wake (adopted child).
(e) Wanandoa wawe wametimiza umri unaokubalika kisheria Mwanamke na mwanamme wawe wametimiza miaka 18 ili kufunga ndoa.
Hata hivyo mwanamke anaweza kuolewa akiwa na umri wa chini ya miaka18 lakini sio chini ya miaka 15 kama atapata idhini
ambayo hutolewa na baba na kama hayupo ni mama au kama wote wamefariki idhini itatolewa na mlezi wa binti huyo.
Itaendelea….