Wananchi
wa Uingereza bado wapo katika majonzi ya timu yao ya taifa kuondolewa
katika mashindano ya Uefa Euro 2016 na Iceland kwa kichapo cha goli 2-1
katika hatua ya 16, hali hiyo ni tofauti kwa nahodha wa zamani wa timu
hiyo, John Terry.
Kupitia
akaunti yake ya Twitter, Terry ameweka picha akiwa na mke wake katika
moja ya fukwe zilizopo Uingereza na kuweka picha zingine akiwa ‘gym’
akifanya mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa 2016/2017.
Terry
ambye kwasasa ana miaka 35 anataraji kuwepo katika kikosi cha Chelsea
cha msimu ujao baada ya kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja na kocha mpya
wa Chelsea, Antonie Conte.


Blogger Comment
Facebook Comment