Wataalamu
wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), wanatarajiwa
kutua nchini wakati wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kukagua Uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza.
Huu
ni utaratibu wa CAF ambako baada ya muda hutembelea nchi wanachama
kuangalia maendeleo ya miundombinu ya mpira wa miguu kabla ya kupandisha
hadhi ya viwanja kwa ajili ya michuano ya kimataifa inayosimamiwa na
kuendeshwa na CECAFA, CAF na FIFA.
Ukaguzi
huo unafanyika wakati Tanzania inasubiri majibu ya Uwanja wa Sokoine wa
Mbeya ambao ulikwiisha kukaguliwa na mapendekezo ya uboreshwaji
kutolewa ili uweze kupandishwa hadhi ya matumizi ya kuchezwa mechi kubwa
kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani, michuano ya
Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na
mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA.
Viwanja
ambavyo CAF na FIFA inavitambua nchini Tanzania hadi sasa ni Amani wa
Unguja, Zanzibar; Kaitaba wa Kagera, Azam Complex na Uwanja Mkuu wa
Taifa vya Dar es Salaam.
Endapo
CCM Kirumba utapitishwa, kutakuwa na nafasi ya kuruhusu kuchezwa mechi
kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani pamoja na
mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na
FIFA.
Kirumba
inaingia kwenye orodha ya viwanja vya Gombani ulioko Pemba; Sokoine wa
Mbeya, Kaitaba wa Kagera ambavyo vilikwisha kukaguliwa na sasa
vinasubiri kupitishwa ili kutumika kimataifa. Ujio wa viwanja hivyo,
utapanua wigo wa Tanzania kuandaa michuano mikubwa katika ngazi ya timu
za taifa kimataifa.


0 comments :
Post a Comment