aturday, July 30, 2016
WAZIRI
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani), amewaonya
wananchi wanaotaka kuvamia njia, litakapopita bomba la mafuta kutoka
Hoima nchini Uganda hadi katika bandari ya Tanga, kwa kujenga nyumba ili
kulipwa fidia mradi utakapoanza.
Aliwaeleza
kuwa bomba hilo lililopewa jina la East Africa Crude Oil Pipeline,
watakaovamia wanapoteza fedha zao na itakula kwao, kwani watatumia
ramani ya satelaiti iliyopigwa Juni mwaka jana, muda ambao mazungumzo ya
ujenzi wa bomba hilo yalianza.
Akizungumza
katika mkutano wa makatibu wakuu wa wizara zote pamoja na wakuu wa
mikoa ambao bomba hilo linapita, Muhongo alieleza kuwa watu hao hawawezi
kudanganya kwa lengo la kupata fedha wakidai kuwa bomba limewakuta.
Alisema
kuna satelaiti 1007 zinazofanya utafiti duniani na mpaka Agosti mwaka
jana, zilikuwa zote zikifanya kazi hivyo kuonesha ni majengo gani
yalikuwepo katika njia hiyo, hivyo kutaka wananchi wapewe ramani
inayoonesha bomba litakapopita ili kuepusha gharama.
Muhongo
alisema leo atakutana na waziri wa Nishati wa Kongo kwa lengo la
kujadiliana jinsi nchi hiyo itakavyoshirikishwa kwenye mradi huo mapema,
huku akitarajia nchi ya Burundi kuungana katika mradi huo.
Alisema hatua hiyo itawezesha bomba hilo kutumiwa na nchi hizo kupitisha mafuta.
Burundi
na Tanzania zinaendelea na utafiti katika ziwa Tanganyika na
yakipatikana watatumia bomba hilo. Muhongo alisema pia wanatarajia
kutumia bomba hilo kusafirisha mafuta kutoka Sudani kusini kutokana na
kuwa ni rahisi kuyasafirisha mpaka Uganda na kutumia bomba hilo.
Bomba
hilo la mafuta linatara kutumia Dola za Marekani bilioni 3.5 mpaka
litakapokamilika na kutaka katibu mkuu kuunda kamati maalumu ya kudumu
ambayo itakuwa na wajumbe wawili au watatu kutoka kila wizara
kuhakikisha mradi huo unakamilika.



Blogger Comment
Facebook Comment