Mashindano
ya Uefa Euro 2016 yanafikia tamati leo kwa mchezo wa fainali kati ya
Ureno na Ufaransa ambao ndiyo waandaji wa mashindano hayo kwa mwaka huu,
mchezo utakaopigwa saa 4 usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki.
Mo Blog imekuandalia mambo 11 ambayo yawezekana ukawa hujayajua kuhusu mashindano ya mwaka huu.
Mashindano ya Uefa Euro 2016 yameshirikisha timu 24
Michezo imefanyika katika viwanja 10
Mpaka sasa imeshachezwa michezo 50
Magoli 107 yameshafungwa na kukiwa na wastani wa magoli 2.14 kwa kila mchezo
Mpaka
sasa watazamaji milioni 2,351,435 wameingia kuangalia michezo hiyo 50
na kukiwa na wastani wa watazamaji 47,029 kwa kila mchezo.
Kuelekea mchezo wa fainali Antoine Griezmann ndiyo anaongoza kwa kufunga magoli mengi akiwa na magoli 6.
Jumla ya Dola Milioni 301 zimetumika katika mashindano ya mwaka huu kwa timu zinazoshiriki;
– Mshindi wa kwanza atapatiwa Dola Milioni 8
– Mshindi wa pili atapatiwa Dola Milioni 5
– Kila timu iliyofika nusu fainali inapatiwa Dola Milioni 4
– Kila timu iliyofika hatua ya robo fainali inapatiwa Dola Milioni 2.5
– Kila timu iliyofika hatua ya 16 bora inapatiwa Dola Milioni 1.5
– Kila timu iliyokuwa ikishinda mchezo katika hatua ya makundi inapatiwa Dola Milioni 1
– Kila timu iliyokuwa inatoa sare mchezo wa hatua ya makundi inapatiwa Dola 500,000
Katika mashindano ya mwaka huu Eden Hazard anaongoza kwa kutoa pasi nyingi za magoli – 4
Mchezaji ambaye amekimbia umbali mkubwa zaidi ni Kingsley Coman wa timu ya Ufaransa, amekimbia Kil. 32.8
Mchezaji
mdogo ambaye ameshiriki mashindano ya mwaka huu ni Renato Sanchez
anayechezea Ureno akiwa na umri wa miaka 18, alizaliwa Agosti 18, 1997.
Aidha katika mashindano ya mwaka huu, Cristiano Ronaldo amevunja rekodi ya Michel Platini ya kufunga magoli mengi katika mashindano ya Euro baada ya kufikisha magoli 9 sawa na Platini.


Blogger Comment
Facebook Comment