SIKU
kadhaa baada ya kuanza kwa kambi ya mazoezi kwa ajili ya matayarisho
ya msimu mpya tayari imethibitishwa kuwa kikosi cha Mbeya City fc kitasafiri mpaka mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri julai 30.
Kwa mujibu wa kiongozi wa Kanisa la Faith Baptist, Mch Jerry Wyatt ambaye
ndiye mwandaaji na msimamizi mkuu wa mchezo huo,maandalizi yote ya
mechi hiyo ya kirafiki itakayoambatana na tamasha kubwa la mahubiri ya
neno la Mungu tayari yamekamilika ikiwa ni pamoja na timu zote
kuthibitisha kuhudhuria.
“Maandalizi
yote yamekamilika, timu zote zimethibitisha kushiriki katika mchezo huo
ambao utaambana na mahubiri ya neno la Mungu kwenye uwanja wa Jamhuri,
naomba watu wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia mchezo mzuri wa
kirafiki kutoka kwa timu hizi mbili pia kupata mahubiri mazuri ya neno
la Mungu sambamba na matukio mengine mengi” alisema.
Akiendelea
zaidi Mch Jerry alisema kuwa kwenye tamasha hilo la neno la Mungu na
mchezo wa kirafiki wa soka hakutakuwa na kiingilio chochote kwa
watakaofika kwenye uwanja wa Jamhuri na kwa wale watakaopata nafasi
wanakaribishwa kuhudhuria ibada kwenye kanisa la Faith Baptist lililopo
Kola B siku jumapili ya julai 31.
“Hakutakuwa
na kiingilio, pia wale watakaopata nafasi nawakaribisha kuhudhuria
ibada kwenye kanisa letu siku ya Jumapili siku ambayo pia tutatoa
zawadi mbalimbali kwa timu za soka zaidi ya 40 za mjini hapa (Morogoro)
kwa maana hiyo litakuwa jambo jema watu wote wakihudhuria”
Hii
ni mara ya pili kwa Mtibwa na City kucheza mchezo wa kirafiki
ulioandaliwa na Kanisa hilo awali ikiwa ni msimu uliopia ambapo timu
hiyo kutoka Manungu iliibuka na ushindai wa bao 1-0 lililofungwa kipindi
cha pili na Mohamed Ibrahim
City inatarajia kuondoka Mbeya Julai 28 tayari kwa mchezo huo uliopangwa kupigwa siku jumamosi ya mwisho wa mwezi huo.
Blogger Comment
Facebook Comment