WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Temeke kuondoa
wafanyakazi wa mkataba kwa anjia ya kuwapa ajira ya kudumu kwa wenye
sifa na kuwaondoa wasiokuwa na sifa ifikapo Julai 30 mwaka huu.
Amesema
kitendo cha kutowaajiri na kuwatumikisha kwa mikataba kwa muda mrefu
kinasababisha wakose stahiki zao jambo ambalo si halikubaliki.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Julai 28, 2016) wakati
akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo na kusisitiza kwamba ni
lazima sula hilo lishughulikiwe haraka kwa sababu hayo ndio matundu
watumishi hewa.
“Mnawatumikisha
watu kama vibarua kwa muda mrefu, hapa kuna wengine wanafanya kazi kwa
mikataba kwa miaka mitano hadi sita hii haikubaliki kwani mnawakosesha
stahili zao pale mnapowaachisha kazi,” amesema.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Temeke kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijiniDar es salam Julai
28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Awali
Kaimu Ofisa Utumishi wa Manispaa hiyo Zaitun Hassan alisema wamekuwa
wakitoa ajira za mikataba kwa sababu wamekosa watu wenye sifa za kuweza
kuajiriwa husan madereva.
“Kwa
mara ya mwisho umetangaza lini nafasi za ajira? Katika mkoa wa Dar es
Salaam kweli wanaweza kukosekana madereva wenye sifa za kuajiriwa?
Alihoji Waziri Mkuu.
Zaitun
alisema kuwa madereva wengi wanaojitokeza pindi wanapotangaza ajira
wanashindwa kufikia vigezo ikiwemo kuwa na cheti cha VETA na badala yake
wanakuwa na cheti cha kidato cha nne tu.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa kuna wafanyakazi wengine katika Idara
ya Uhasibu na Ujenzi ambao nao wameajiriwa kwa mkataba hivyo amemtaka
Ofisa Utumishi kuomba kibali cha kuajiri kwa Katibu Mkuu Utumishi.
Baadhi
ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa
Halmashauri hiyo jijini Dar es salaam Julai 28, 2016
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda kufanya tathmini ya maeneo yote ya shule kwenye mkoa wake
na watakaobainika kuingia katika maeneo hayo waondolewe haraka.
Amesema
baada ya kukamilisha utengenezaji wa madawati kinachofuatia sasa ni
ujenzi wa vyumba vya madarasa, ambapo amezitaka halmashauri kuweka
mipango ya kujenga majengo ya madarasa ya ghorofa ili waweze kuwa na
madarasa mengi katika eneo dogo.
Awali
Waziri Mkuu alipokea msaada wa madawati 705 katika hafla iliyofanyika
kwenye viwanja vya shule ya msingi Chamazi wilayani Temeke ambapo kati
yake Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania umetoa madawati 600 na Jumuia ya
Mabohora imetoa madawati 105.
Pia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk.
Agustino Mahiga alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 85 fedha
zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo kwa ajili ya kuchangia
utengenezaji wa madawati.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa mkoa wa Dar es salaam
baada ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Temeke
kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijini Dar es slaam Julai 28, 2016.
Dk.
Mahija alisema watumishi hao walichanga sh. milioni 100 kwa ajili ya
utengenezaji wa madawati ambapo sh. milioni 15 wamekabidhi kwa mkuu wa
wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe ambaye alikuwa mtumishi wa wizara hiyo
ili naye akatengeneze madawati kwa shule za wilayani kwake.
Kwa
upande wake Balozi wa Kuwait nchini Jaseem Al Najem amesema Serikali ya
Kuwait itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika shughuli
zote za maendeleo hususan katika sekta za elimu na afya.


Blogger Comment
Facebook Comment