Chama cha upinzani chapinga matokeo ya urais mahakamani Zambia

Bwana Hichilema anasema kuwa ushindi wake uliibwa

Image captionBwana Hichilema anasema kuwa ushindi wake uliibwa
Chama kikuu cha upinzani nchini Zambia kimepeleka kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Edgar Lungu uliofanyika mapema mwezi huu.
Mgombea wake wa urais Hakainde Hichelema, aliiambia BBC kuwa uchaguzi huo uliibwa kutoka kwake na haukuonyesha matakwa ya watu wa nchi humo.
Chama chake cha National Development (UNDP) kimemuandikia spika wa bunge, kikimtaka achukue wadhifa wa urais hadi uamuzi wa mahakama utolewe.
Tume ya uchaguzi nchini Zambia ilikuwa imemtangaza Lungu kuwa mshindi kwa asilimia 50.35 huku Hichilema akipata asilimia 47.67 na kusisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki.
Bwana Lungu alimshinda Hichilema uchaguzi uliotangulia mwaka uliopita kwa chini ya kura 28,000.
Chanzo:BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment