Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla amefanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kufuatia taarifa zilizoripotiwa kwenye mitandao ya Kijamii na
baadhi ya Magazeti ya hapa Nchini juu ya kutelekezwa bila kupatiwa
huduma kwa mgonjwa wa Sickle Cell (Selimundu) na Madaktari na manesi wa
Hospitali hiyo.
Dk.
Kigwangalla ameweza kufika kwenye Hospitali hiyo ya Muhimbili na
kisha kwenda moja kwa moja kwa mgonjwa huyo ambaye awali picha yake
ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ujumbe wa kutelekezwa
iliyosambazwa na Wanaharakati wa Sickle Cell ambao waliomba Serikali
ichukue hatua. (Kama walivyoandika kawenye ujumbe hapa chini).
Hata
hivyo, Dk. Kigwangalla baada ya kujionea hali halisi ya tukio la
mgonjwa huyo kupitia mitandao na magazeti aliamua kutembelea mwenyewe
katika wodi ya magonjwa ya damu (Haematology) huku akiomba kuoitia
nyaraka zake zote pamoja na kupatiwa taarifa za kutelekezwa mgonjwa huyo
kama ilivyoripotiwa ambapo hata hivyo hali ilikuwa ni tofauti na
ilivyoripotiwa.
“Nimekuja
mwenyewe na wala sikutaka kutuma wasaidizi wangu. Nimemtembelea Mgonjwa
‘KK ‘ na kukuta hajatelekezwa wala kunyanyaswa. Hajalazwa chini.
Ameonwa na jopo la Madaktari bingwa lililoongozwa na Dk. Stella, kwa
siku mbili mfululizo tokea alipowasili wodini.
Mgonjwa
alilazwa juzi. Ni kweli anaumwa Sickle Cell, yupo kwenye ‘painful
crisis’, lakini amepewa Antipains zote anazopaswa kupewa ikiwemo kali
kabisa ya aina ya ‘Morphine’! Mgonjwa hana malalamiko. Mwanzoni hakujua
mimi ni nani na nilikuwa peke yangu na hivyo hakuogopa kunipa taarifa
yoyote ile. Pia nimekagua faili lake neno Kwa neno, nimeridhika
ametibiwa ipasavyo.
Kuzusha
taarifa za uongo, kutafuta ‘sympathy’ (huruma) Kwa kusingizia watu
kunakatisha tamaa, Hivyo naagiza Hospitali zote nchini kudhibiti wageni
kupiga picha wodini hii ni pamoja na kuzuia simu zote za camera
kuingizwa mawodini pamoja na camera za aina yoyote ile na kwa
atakayekihuka kuna sheria na kanuni zitafanya kazi” alieleza Dk.
Kigwangalla.
Kwa
upande wake mgonjwa huyo Mwanadada, K. Kasongo ambaye alikiri kufika
hapo siku tatu zilizopita na kupokelewa vizuri na wahudumu pamoja na
Madaktari ambapo na kupatiwa huduma stahiki.
Kwa hali hiyo, Dk. Kigwangalla aliomba jamii kuacha kuripoti mambo wasiyo yajua kwani yanaweza kuchangia upotevu wa amani.
“Nilisononeka
sana awali wakati nimepata habari hizi. Bahati mbaya nilikuwa Jimboni,
sikuwa na namna ya kufanya zaidi ya kurudi Ofisini kisha kufuatilia.
Niliyoyakuta hayafanani hata chembe na kilichoandikwa hapa na
wanaharakati hawa wa Sickle Cell (selimundu). Wakati tukihangaika
kuboresha huduma za Afya nchini Kwa ajili ya watu wote, Wakati tukifanya
kazi Kwa bidii zote, usiku na mchana, masaa ya ziada, Kila kona ya
nchi, kutwa kucha barabarani, unakutana na watu wa aina hii, wanapotosha
umma, wanaotafuta umaarufu wa taasisi yao kwa kutoa taarifa za uongo
kwa umma juu ya mambo wasiyoyajua. Alieleza Dk. Kigwangalla.
Aidha,
aliongeza kuwa: kutokana na hali hiyo ambayo imeonekana kukatisha sana
tama, ametoa rai kwa Wanaharakati kutambua kuwa Serikali imewekwa
madarakani na wananchi kwa kura na Kwa Msingi huo ina imani na Matumaini
kamili ya wananchi, Na pia ina uchungu na huruma kwa wananchi walioipa
mamlaka na si vinginevyo.
Na
kwamba, hata siku moja wanaharakati wasidhani wanaweza kuwa mbadala
kamili wa Serikali, wao ni wabia muhimu na wanaisaidia Serikali
kuutumikia umma (complementary efforts) na Siyo mbadala (alternative) wa
Serikali. Kama wabia wakuu wa Serikali, wanaharakati wana wajibu wa
kusema ukweli bila kuegemea upande wowote ule ili kulinda heshima yao na
kulinda ‘relevance’ yao kwenye mfumo wa uongozi na utawala wa nchi.


0 comments :
Post a Comment