Lowassa atembelea shule iliyoungua moto Arusha


Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA jana alitembelea shule ya Nanja iliyoungua moto hivi karibuni mkoani Arusha.

Akiambatana na viongozi wengine katika jimbo la Monduli Lowassa aliwataka viongozi kuhakikisha shule za bweni zinajengwa vizuri na kuwekewa mifumo ya kujikinga na ajali za moto kama ambavyo sasa shule tano kwa kipindi kifupi zimeungua moto mkoani Arusha na chanzo kikiwa hakijulikani.

“Napenda kuwakumbusha wakuu wa shule na viongozi kwamba ni muhimu shule zote za mabweni ziwezeshwe na zijengwe vizuri huku zikichukuliwa tahadhari zote za kujikinga na ajali kama hizi, pia nitaungana na uongozi wa jimbo la Monduli pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha shule hii inarekebishwa na watoto wanarejea katika mabweni” Alisema Lowassa.

Aidha Lowassa alitumia nafasi hiyo kuwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii kwani elimu ndiyo mkombozi wa maisha yao.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment