Mchezo
wa ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kati yaLeicester
City na Manchester United umeifanya Man United kuzidi kujiwekea hitoria
nzuri ya kutwaa taji hilo baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Furaha
ya Manchester United ambayo iliwekwa na Jesse Lingard na Zlatan
Ibrahimovic imeifanya Manchester kuwa timu yenye mafanikio makubwa zaidi
katika kushinda kikombe hicho kwa kufikisha vikombe 21 rekodi ambayo
haijafikiwa na vilabu vingine, Liverpool ikishika nafasi ya pili na
vikombe 15, Arsenal nafasi ya tatu na vikombe 14.
Hata
hivyo pamoja na kuibuka na ushindi huo, kocha wa Man United, Jose
Mourinho amesema ushindi wa mchezo wa ngao ya jamii na kutwaa ubingwa
anautoa kwa aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Louis Van Gaal kwani ndiye
aliyewawezesha kupata nafasi ya kucheza mchezo huo.
“Ushindi
huu ninautoa kwa Mr. Van Gaal na kwa wachezaji saba ambao niliacha
kuwapanga katika mchezo wa Leicester, Van Gaal ndiye ambaye ametufanya
kupata nafasi ya kucheza huu mchezo bila yeye tusingepata hii nafasi
namshukuru sana kwa hilo,
“Kwa
wachezaji niliowaacha haikuwa na jinsi ni lazima nifanye maamuzi lakini
bila kuwa Depay, Jones, na Ashley Young katika benchi sio jambo rahisi
lakini ilibidi kufanya hivyo na huu ushindi ninautoa kwao,” alisema
Mourinho.


0 comments :
Post a Comment