Siku
kadhaa baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kurejea kutoka katika
matibabu India, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemtembelea
nyumbani kwake kwa ajili ya kumjulia hali.
Kiongozi
wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akisalimiana na
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar
es Salaam.Spika wa Bunge amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini
India alipokwenda kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe aliyemtembelea Nyumbani kwake Jijini
Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Bunge).
0 comments :
Post a Comment