Wekundu wa Msimbazi Simba Sport Club leo inashuka dimbani katika mchezo wake wa pili dhidi ya JKT Ruvu mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Simb SC inashuka dimbani ikiwa na pointi tatu muhimu baada ya mchezo wake wa awali kushinda dhidi ya Ndanda kwa ushindi wa bao 3-1. Simba Sc na JKT Ruvu ni miongoni mwa timu zenye kukamiana zinapokutana uwanjani hivyo mchezo wa leo utakuwa ni wa aina yake.
Mbali na Simba na JKT Ruvu, michezo mingine itakayochezwa leo ni pamoja na:
Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Manungu, Morogoro, Azam wataikaribisha Maji Maji na Prisons watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Timu ya Mbao watakuwa wenyeji wa Mwadui FC Uwanja wa Kirumba, Mwanza, Kagera Sugar watamenyana na Stand United Uwanja wa Kambarage, wakati mabingwa watetezi, Yanga SC watacheza mechi ya kwanza kesho kwa kumenyana na African Lyon, siku ambayo pia Toto Africans watakuwa wenyeji wa Mbeya City Kirumba, Mwanza.
Msimamo wa Ligi baada ya mechi za ufunguzi juma lililopita
0 comments :
Post a Comment